Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele akimkakabidhi mkoba wenye fomu za kuomba kuteuliwa kuwa Mgombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF), Mhe. Gombo Samandito Gombo.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume, Ndg. Ramadhani Kailima akimuelekeza namna ya kujaza kitabu Mgombea wa kiti cha Rais kutoka Chama cha Wananchi (CUF), Mhe. Gombo Samandito Gombo.
Mgombea wa kiti cha Rais kutoka Chama cha Wananchi (CUF), Gombo Samandito Gombo akijaza kitabu kuonesha amekabidhiwa fomu hizo.
Mgombea Mwenza, Mhe. Husna Mohamed Abdalla akaisaini kitabu.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume, Ndg. Kailima Ramadhani akizungumza wakati wa utoaji huo wa fomu.
Wanachama wa CUF wakiwa ukumbini kushuhudia utoaji wa fomu za uteuzi kwa wagombea wa chama chao.