Na Magrethy Katengu,Jamhuri Media
Dar es Salaam

Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, amewataka viongozi wa vyama vya siasa nchini kuhakikisha kampeni za Uchaguzi Mkuu wa 2025 zinafanyika kwa kistaarabu, bila kutumia lugha za matusi, kashfa au vitendo vyovyote vinavyoweza kuhatarisha tunu ya amani Taifa iliyopo

Amesema hayo Jijini Dar es Salaam Agosti 18, 2025, wakati akifungua Mafunzo kuhusu Sheria ya Gharama za Uchaguzi kwa Viongozi wa Kitaifa wa Vyama vya Siasa ambapo amesisitiza kuwa vyama vya siasa vina wajibu wa kuendeleza misingi ya amani na mshikamano wa taifa.

“Nendeni mkafanye kampeni za kistaarabu mkiwanadi wagombea wenu. Jiepusheni kabisa na lugha za matusi, kashfa, uchochezi au vitendo vyovyote vinavyoweza kuvuruga amani na utulivu wa taifa letu,” amesema Jaji Mutungi.

Ameongeza kuwa amani na mshikamano ni urithi ulioachwa na waasisi wa taifa, hivyo viongozi wa kisiasa wanapaswa kuwa mfano wa kuigwa kwa wananchi.

“Kumbukeni kuna maisha baada ya uchaguzi. Uchaguzi si mwisho wa siasa wala maendeleo. Turithishe amani hii kwa kizazi hiki na vizazi vijavyo,” amesema” Jaji Mitungi.

Sambamba na hayo amewasihi , viongozi kutokubabaishwa na upotoshaji unaoweza kusambazwa kupitia mitandao ya kijamii na makundi mengine katika jamii akisisitiza kuwa uchaguzi utafanyika kama ulivyopangwa taarifa zinazoleta taharuki wawe nazo makini.

“Mtaambiwa uchaguzi haupo, msikate tamaa. Uchaguzi upo, na jambo kubwa zaidi ni kuhakikisha tunaingia kwenye uchaguzi huru na wa haki kwani ninyi ndio wakala wa kwanza wa kuhakikisha hilo linatekelezeka,” amehimiza.

Kwa Upande Mwasilishaji Kuhusu Sheria Wakili Edmumdi Mgasha Amebainisha kuwa Kifungu cha kanuni za Uchaguzi 6(,1)(2) kinamtaka Msajili kuweka pingamizi dhidi ya Mgombea aliyeshindwa kuweka Wazi kiasi cha vyanzo vya gharama za Uchaguzi ndani ya siku 14 baada ya uteuzi