Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Kahama
MWENYEKITI wa Tanzania Mzalendo Foundation Bw. Khamis Mgeja ameishauri na kuiomba wizara ya elimu nchini ifikilie kuona umuhimu namna gani ya kuweza kuanzisha masomo ya aman, Uzalendo na mazingira mashuleni kuanzia madarasa ya awali mpaka vyuo vikuu.
Mgeja mabaye anasimamia taasisi inayojishughulisha na masuala ya haki, Amani na Demokrasia Nchini yenye makao makuu yake mjini Kahama ametoa ushauri huo alipokuwa mgeni Rasmi katika sherehe ya mahafali ya kwanza ya darasa la awali na darasa la saba katika shule ya msingi AL WAHAAB PRE, AND PRIMARY SCHOOL iliyopo mtaa wa Sango Manispaa ya Kahama Mkoani Shinyanga.
Mgeja amesema suala la amani Uzalendo na mazingira ni suala muhimu sana katika ustawi wan chi na usalama pia uchumi na maendeleo endelevu kwani watoto wakifundishwa tangia wakiwa watoto wadogo watajengeka na kuwa na utamaduni katika kuyaishi maisha yao ya kila siku kwani utamaduni unajengwa hauoti kama uyoga na waswahili wanausemi “samaki mkunje angali mbichi” alisema Mgeja.

Mgeja aliendelea kusema kuwa chokochoko zote zinazotokea kote Duniani za uvunjifu wa amani na ukosefu wa uzalendo ni tatizo la jamii ambayo haikuandalika vizuri na kujua thamani ya amani, Uzalendo na mazingira.
Mwenyekiti huyo wa Tanzania Mzalendo Foundation alisema Tanzania bado hatujachelewa kuelimishana umuhimu na thamani ya amani, Uzalendo na mazingiira japo kuna viashilia vimeanza kujitokeza kidogokidogo kwa baadhi ya watanzania wenzetu waliolewa amani na kuvimbewa wanaanza kujaribu kutikisa amani iliyopo lakini kikundi hicho cha wachache kinajidanganya hakitaweza kuichezea amani kwani nchi yetu iko salama katika uongozi imara kwa mama yetu Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Vile vile Mgeja alimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuiongoza nchi vizuri na kuhakikisha kuwa nchi yetu inakuwa na amani na nchi iko katika mikono salama chini ya uongozi wake wa serikali ya awamu ya sita na kutumia nafasi hiyo kuwaomba watanzania kuendelea kumuunga mkono katika kudumisha amani na kujiletea maendeleo.
Aidha Mgeja aliwapongeza viongozi wa Dini nchini kwa kuendelea kuwahamasishwa waumini wao na watanzania kwa ujumla umuhimu wa kuitunza amani yetu kama mboni ya jicho, na kwamba wanastahili pongezi kubwa sana viongozi hao wa Dini wa madhehebu mbalimbali.

Kuhusu suala la elimu Mgeja alizipongeza sekta binafsi na taasisi za dini kwa kushilikiana na serikali kuendelea kuwekeza katika elimu kwani katika dunia ya sasa ya sayansi na teknolojia elimu ni muhimu kuwekeza kwa watu wetu kwani kama tunahitaji mafanikio kwa haraka sayansi inahitajika kuwekezwa kila mahala na hasa katika masuala ya kilimo, Ufugaji, Uvuvi, Ufundi Biashara na Viwanda na mpaka kwenye sekta ya Madini kwamba kote huko kuna hitaji sayansi ya hali ya juu sana ili kuweza kupatikana kwa tija kubwa yenye mafanikio makubwa.
Kuhusu mabadiliko ya mfumo wa elimu Mgeja alipongeza serikali ya awamu ya sita chini ya mama yetu Rais Dakt. Samia Suluhu Hassan kufanya mabadiliko makubwa kuhusu mfumo huo wa elimu nchini na kuweka mtaala wa amali jambo ambalo litawafanya vijana wetu wapate elimu ya kujitegemea na ujuzi.
“Nawaomba watanzania wenzangu tumuunge mkono Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan kutuletea elimu ya mkombozi,” alisema Mgeja.
Mgeja aliongeza kuwa kuhusu ajira aliwaomba vijana wajitahidi kujiendeleza kiujuzi na kuongeza ufahamu wa lugha za kigeni ambazo ziko sokoni hivi sasa hasa kiingereza, Kichina, Kiarabu na kifaransa kwani lugha hizo kwa sasa zimekuwa ni bidhaa muhimu sana katika mafanikio ya ajira na biashara tusipofanya hivo tutaendelea kuwa watazamaji katika soko la ajira Duniani.
Aliwapongeza wakurugenzi na bodi ya wadhamini shule ya Al Wahaab Muslim kwa kuliona hilo tatizo na kuanza kuliwekea mkakati wa kuanza mpango wa kuongeza na walimu kutoka nje ya nchi kwamba ni jambo jema katika kuunganisha nguvu za kitaaluma.

Kwa upande wao wakurugenzi wa shule ya Al Wahaab Muslimu Shekhe Mohamed Issa Hilal na Ahmed Abdulrahaman Haluna Wakitoa taarifa mbele ya mgeni rasmi Khamis Mgeja ambaye ni mkurugenzi wa Tanzania Mzalendo Foundation na viongozi wa Dini pamoja na wazazi na wanafunzi wa shule hiyo kwanyakati tofauti lisema kuwa shule hiyo ilianzishwa mwa 2019 na mahafari hiyo ni yakwanza tangu kuanzishwa kwake.
Wakurugenzi hao walieleza kuwa shule yao imekuwa na mafanikio makubwa katika malezi mema, Elimu bora na maadili kwamba hii ni dalili tosha kwa mbegu tunayoipanda inakuwa bora na imeendelea kuzaa matunda mema ndani ya jamii ya Kahama na Tanzania kwa ujumla.
Kuhusu mikakati ya shule waakurugenzi hao walisema kuwa tayari wamenunua ekari 60 na wanatarajia kuanza ujenzi wa shule mwaka 2026 ili kuipanua shule pamoja na kujenga mabweni na kuwa viwanja vya micchezo na kuongeza kuwa shule hiyo pia ina mradi wa ufugaji wa mifugo.
Katika Mahafari hayo viongozi wa dini, wakurugenzi wa shule hiyo pamoja na walimu, wazazi na wanafunzi akiwemo mgeni rasmi Khamis Mgeja walihitimisha hafra hiyo kwa kuomba dua kuiombea nchi amani na kumuombea dua ya mafanikio mema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ambae pia ni mgombea Urais kwa tiketi ya CCM.
