Tume ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani yaliyojitokeza wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, leo Januari 22, 2026, imekutana na viongozi wa vyama mbalimbali vya siasa nchini.
Mkutano huo wa Tume na viongozi wa vyama vya siasa nchini umefanyika katika Ukumbi wa Tanganyika uliopo katika ofisi za Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Jijini, Dar es Salaam.
Miongoni mwa yaliyojadiliwa katika kikao hicho ni pamoja na namna matukio hayo yalivyoanza, athari zake kwa watu, mali na miundombinu pia ushauri wa namna ya kuondokana na matukio hayo.
Tume inaendelea kukutana na makundi mbalimbali wakiwemo waathirika wa Matukio hayo na kuyawasilisha kwa ajili ya hatua zaidi.









