Na Aziza Nangwa, JamhuriMedia, Dar es Salaam

Benki ya CRDB imewataka wananchi kuchanja kidital ili kushinda safari ya kwenda kungalia kombe la Dunia

Akizungumza na waandishi wa habari mkurugenzi wa wateja wadogo na wakati Boniventure Paul ,alipokuwa akizindua kampeni ya CRDB finali ndiyo mpango mzima na Tembo card.

Amesema wamekuja kuitambulisha rasmi kampeni hiyo kwa wateja ili kuwawezesha wateja kufanya miamala kwa wingi kwa kutumia mtindo wa kidital na kupunguza mfumo wa cash.

‘’Kampeni hii ni sehemu ya jitihada za benki ya CRDB ,kuendelea kuhamsisha matumizi ya malipo kidigitali kwa kuleta ubunifu katika
huduma za kifedha nchini’’amesema.

Paul amesema wamefanya hivyo kwa wateja , kutokana na uaminifu wao qakaamua kuwa zawadia zawadi ambayo ni zaidi ya mchezo bila kujali tamaduni.

‘’Sisi kama CRDB tumeona, tuwape nafasi wateja wetu kupata sehemu ya msisismko huo wa kimataifa.

Kupitia kampeni hii wateja wetu watapata fursa ya kufurahia ,urafiki na usalama wa kutumia Tembo kadi visa, huku wakipata nafasi ya kushinda zawadi mbalimbali za kuvutia’’amesema

Amesema kampeni hiyo itaendeshwa kwa kipindi cha miezi mitatu, itakwenda mpaka mwezi June katika kipindi hiki cha miezi mitatu wateja wote wenye kadi zetu mbalimbali wataweza kuibuka washindi wakati wowote .

‘’Ili kushirikia mteja anapaswa kutumia miamala walau therasini ,kwa mwezi katika mashine zetu au mtandaoni’’amesema

Amesema kama mteja atafanya miamala miwili au mitatu kwa siku, atajiweka katika nafasi nzuri ya kujishindia safari au TV ya nchi 85 na decoda.

‘’Katika mchakato wa shindano hilo kutakuwa na washindi 20 ,kati yao kumi watakwenda kushudia mechi za kombe la Dunia na kumi watapewa smart TV ya nchi 85 na decoda ili kuhakikisha kwamba huyu ambaye amebakia nyumbani anaangalia mashindano hayo moja kwa moja

Kutakuwa na droo tatu ambapo,washindi wanne wa kwanza watakwenda Marekani kushudia mashindano na watatu watajishindia Tv inch 85 na dekoda itakuwa12 /4/2026

Droo ya pili itafanyaiaka tarehe 12 mwezi wa tano ambayo hii itakuwa na washindi watatu ambao watakwenda Canada na washindi watatu watashinda Tv na decoda

Droo ya mwisho tarehe 11 juni ndiyo ya mwisho itakuwa na washindi saba kati yao , wanne watakwenda Canada na watatu watajishindia Tv na decoda.

Tunatarajia wateja watatumia nafasi hii ,kuendelea kuchanja kwa kutumia Tembo kadi visa hii itatusadia kuoana kwamba wateja wetu wanafanya malipo bila kubeba cash’’amesema.

Amesema mteja atatakiwa kufanya miamala 30 ,kwa mwezi anakuwa katika
katika nafasi nzuri ya kushinda lengo la kuweka hivi tunataka kupunguza matumizi ya cash.