Dar es Salaam inatarajiwa kuwa mwenyeji wa moja ya maonesho makubwa ya kilimo Afrika, Africa Agri Expo (AAE) 2026, yatakayofanyika Septemba 2–3, 2026 katika Viwanja vya Maonesho vya Mwalimu J.K. Nyerere.
Maonesho hayo ya mwaka wa 10 yataenda sambamba na Future Food, Livestock & Poultry Expo (FLIP 2026), yakilenga kuwakutanisha wakulima, wawekezaji, wafanyabiashara, wazalishaji wa teknolojia za kilimo pamoja na wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya Afrika.
Zaidi ya washiriki 10,000 wanatarajiwa kuhudhuria, huku kampuni zaidi ya 1,000 za sekta ya chakula, mifugo na kilimo zikitarajiwa kuwakilishwa kutoka nchi mbalimbali duniani.
Washiriki watapata fursa ya kuona teknolojia mpya za kilimo ikiwemo mashine za kisasa za kilimo, mifumo ya umwagiliaji, teknolojia za ufugaji, mbegu bora, chakula cha mifugo na suluhisho za kuongeza thamani ya mazao.
Aidha, maonesho hayo yatakuwa jukwaa la wafanyabiashara na wawekezaji kupata washirika wapya, mikataba ya usambazaji wa bidhaa, pamoja na kujifunza mikakati ya kukuza biashara katika sekta ya kilimo Afrika Mashariki.
Kwa kuwa Tanzania ina nafasi muhimu katika uzalishaji wa chakula na biashara ya kilimo, waandaaji wanaeleza kuwa Dar es Salaam imechaguliwa kuwa eneo sahihi la kuunganisha fursa za kilimo, mifugo na uwekezaji katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Africa Agri Expo 2026 inatarajiwa kuwa daraja la kuunganisha teknolojia za kimataifa na fursa kubwa za kilimo cha kisasa barani Afrika.
Jisajili kushiriki: 👉 https://africa-agriexpo.com/visitor-registration.html



