-Rais Samia azindua minara 758 kuimarisha Mawasiliano
Na Byarugaba Innocent, ORMV
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan Aprili 10,2026 amezindua Minara 758 maunganisho ya Mkongo wa Mawasiliano katika Wilaya 85 na makabidhiano ya Mkongo wa Mawasiliano Serikalini hafla iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma.
Hii ni fursa nyingine muhimu inayokwenda kuchagiza na kuongeza kasi ya Mawasiliano nchini hasa maeneo ya vijijini kwa kuongeza ajira kwa Vijana na kuinua uchumi wa kidijitali kwa kufanya biashara mtandao na huduma mtandao kupitia sekta ya teknolojia ya Habari na Mawasiliano.
Awali akiwasilisha taarifa fupi ya Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Katibu Mkuu wa hiyo Mohammed Khamis Abdulla amesema Mawasiliano ya 2G,3G na 4G yameboreshwa kwa asilimia huku 5G ambayo mpaka Mwaka 2021 haukiwepo ukifikia asilimia 33.3 hali inayokwenda kuleta mapinduzi makubwa kwenye sekta zote zinazotegemea sekta ya Habari na Teknolojia ya Mawasiliano ikiwemo elimu, huduma za kifedha kupitia biashara mtandao sambamba na kuwa uhakika wa Mawasiliano muda wote yenye gharama nafuu.
Minara 758 inayozinduliwa leo imetumia kiasi cha fedha shilingi 126 bilioni ikijengwa kwenye mikoa 126 ya Tanzania Bara na kuzifikia Wilaya 121 kati ya 139 sawa asilimia 82 ambapo matarajio ni kufikia 100% ifikapo Disemba,2026
Akizungumza na Wananchi kupitia hafla hiyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan ametoa rai kwa wadau kuendelea kushirikiana na serikali katika bunifu za kidigitali ili kuhakikisha hakuna Mtanzania anabaki nyuma katika kuitumia mitandao ya simu kwa manufaa ya kulijenga Taifa, kuimarisha amani, mshikamano na kulinda maadili ya Mtanzania.








