Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine amempendekeza mkuu wa shirika la nishati la serikali la Naftogaz, Sergii Koretskyi, kuwa Waziri Mkuu mpya wa nchi hiyo.
Pendekezo hilo tayari limewasilishwa bungeni ambapo kura inatarajiwa kupigwa mapema leo Alkhamis, kufuatia kujiuzulu kwa Waziri Mkuu Yulia Svyrydenko na serikali yake baada ya kuwa madarakani kwa chini ya mwaka mmoja.
Mabadiliko hayo makubwa yanayolenga kuimarisha uhusiano wa Ukraine na washirika wake wa kimataifa, yanatarajiwa pia kumuondoa Waziri wa Ulinzi, Mykhailo Fedorov, ambaye anaripotiwa kuwa na mzozo na wakuu wa jeshi.
Hii itakuwa mara ya pili kwa Ukraine kubadilisha Waziri Mkuu na mara ya nne kubadilisha Waziri wa Ulinzi tangu Urusi ilipoivamia nchi hiyo kijeshi mwaka 2022.



