Shule ni taasisi muhimu kwa watoto kukuzwa kiafya ya akili na mazingira, kila mzazi anapompoleka mtoto shule huwa anajukumu la kuhakikisha mahitaji muhimu ya kujifunzia ikiwemo, sare za shule, daftari karamu na mahitaji mengine mtambuka.


Walimu hutimiza majukumu yao kwa mujibu wa taaluma na miongozo ya serikali katika taaluma hiyo
Kimsingi walimu niwatu muhimu sana kwa malezi ya watoto shuleni na jukumu lao kwa kiasi kikubwa wana lifanya kwa weledi na umakini mkubwa sote nimashaidi kuwa serikali imeweka miongozo kwa tasasi za elimu ili kuhakikisha watoto wana pata elimu inayoendana na soko la dunia na mahitaji ya wakati.
wajibu wa wazazi;

  1. Kuhakikisha mahitaji ya mtoto
  2. Kufuatilia kwa ukaribu daftari au mafunzo mtoto anayopata
  3. Kumsaidia mtoto kumaliza kazi alizo pew ana mwalimu
  4. Kumpa moyo mtoto ili azidi kujitahidi katika kushika elimu
  5. Kushiriki vikao vya wazazi shuleni
  6. Kutoa michango inayohitajika shuleni mfano ulinzi, au chakula cha watoto

Wajibu wa walimu
1 Kufundisha masomo kwa mujibu wa miongozo na ithibati ya elimu
2 Kusimamia nidhamu na mwenendo wa Watoto wawapo shuleni

Umuhimu wa kuwatembelea watoto shuleni
1 Inaonyesha moyo wa kujari mtoto hata walimu wanaowafundisha
2 Inaongeza hari ya kujiamini kwa mtoto
3 Inatengeneza uhusiano mzuri kati ya mtoto na mzazi
4 Inasaidia mzazi kujua mahitaji ya zaidi ya mtoto kwa kupata taarifa za ziada toka kwa mwalimu au wakufunzi
5 Inapunguza mashaka juu ya mwenendo au tabia ya mwanafunzi
6 Inasaidia kuwapa morali walimu kushirikaiana na wazazi katika swala zima la malezi

HITIMISHO
Kiukweli wazazi tunapo kuwa tumewa kabidhi Watoto wetu kwa walimu tuna hisi kama tumesha tua mzigo wa malezi na kuwaachia walimu hili suala si sawa kabisa, wazazi tunapaswa kuwa na utaratibu wa kuwatembelea waotot wetu wanapokuwa shule si tu katika ngazi ya msingi hata katika sekondari na taasisi za elimu ya juu, tukiwa na hii desturi itakuwa njema katika malezi ya watoto

Imeandaliwa na John Francis Haule, Mkuu wa soko la Samunge jijini Arusha
SIMU 0756717987 au 0711993907