Na Aziza Nangwa, JamhuriMedia, Dar es Salaam
Shirika lisilo la kiserikali la Active African Women in Research and Development (AAWORD) ,limetoa mafunzo ya utunzaji wa mazingira kwa wanafunzi zaidi ya 50 kutoka katika shule ya sekondari Keko
Akizungumza na wakati wa mafunzo wezeshaji wa mafunzo hayo ,Dkt Gladness Munuo ambaye pia ni mwanahabari mkongwe na mkobezi katika masuala mbalimbali ya ikiwemo jinsia afya ya jamii na mshauri amesema elimu hiyo ni muhimu kwa vijana hao kwasababu wataweza kujifunza vyema juu ya utunzaji wa mazingira hasa maji yanayo tililika kutoka viwandani
Dkt Gladness amesema wanafunzi hao wakijifunza vizuri juu ya utunzaji wa mazingira na madhara ya utililishaji maji machafu ya viwandani ni wazi watakuwa mabalozi wa kukemea Suala hili katika jamii ikiwemo mazingira yanayowazunguka
Amesema amejinga na shirika hilo, ili kuongeza chachu ya uhamasishaji wa Suala zima la utunzaji wa mazingira katika jamii
Amesema vijana wanapo patiwa elimu ,ya mazingira hasa wakiwa shuleni wanatia hamasa kwa wenzao kujiunga katika mapambano juu ya utunzaji mazingira yanayowazunguka
Fatuma Kikwape Mwenyekiti wa kikundi chaa mazingira kata ya Keko amesema kwa sasa elimu ya mazingira ni muhimu kutokana na ukuaji wa viwanda katika eneo lao lao.
“Wakati tunaanza kampeni zetu za utunzaji wa mazingira , hali ilikuwa mbaya elimu kwa jamii ilikuwa bado mpaka tulipo fikiwa na shirika AAWORD watu walikuwa wakiugua magonjwa ya ngozi kutokana na kutumia maji yasio salama.
Amesema baada ya kupewa elimu, jamii iliona umuhimu wa kuepuka uchafuzi wa mazingira na kuwezesha kasi ya magonjwa kupungua”Amesema.
Amesema kwasasa shirika hilo limemua kuelimisha wanafunzi, hatua ambayo ameipongeza na kudai itaongeza nguvu ya utunzaji mazingira miongono mwa vijana kuona umuhimu wake.
Mwalimu Fortunes Sangana wa sekondari ya Keko amesema ,mradi huo ni muhimu sana kwa wanafunzi kwani utawasadia kutunza mazingira yao na kuwa mabalozi katika jamii kwani ni muhimu katika kujenga taifa lenye afya Bora
Amesema ni vyema wadau wengine, wakajitokeza kwenda katika shule hiyo kusadia kutoa elimu juu ya changamoto mbalimbali za mazingira na nyingine zinazowakabili
Amesema viwanda vimekuwa mstali wa mbele katika kuchafua mazingira katika eneo hilo ,hivyo elimu walioyo ipata Wanafunzi itawasaidia kufanya vyema katika kusimamamia Suala zima la uchafunzi wa mazingira ya maji katika maeneo yao.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa shirika hilo Idda Swai amesema AAWORD imeanzishwa kwa ajili ya kutoa mchango katika maendeleo ya kijamii, uchumi na mazingira kupitia tafiti zinazo lenga kuleta mabadiliko utetezi wa sera,ujenzi wa uwezo wa Wanawake na vijana pamoja na utekelezaji wa miradi inayo chochea maendeleo endelevu
“Shirika linafanya kazi na Serikali ,Taasisi za umma na sekta binafsi ,washirika wa maendeleo ndani na nje ya nchi pamoja na asasi za kiraia lengo ni kuhakikosha wanawake,vijana na makundi yaliyo katika mazingira magumu wanapata fursa sawa kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya taifa
Idda amesema katika kutekeleza shughuli zake wamekuwa wakizingatia ,misingi ya haki za binadamu usawa wa kijinsia uwajibikaji ,ushirikisheaji,uwazi,uadilifuna maendeleo endelevu inayoendana na dira ta Taifa
“Kwa sasa malengo yeti ni kutetea na kuendeleza haki za kijamii,kiuchumi,kisiasa na Sheria za wanawake,vijana na makundi maalum”Amesema
Amesema kama shirika wamejizatiti kujenga harakati imara za wanawake nchini ,ambapo kupitia tafiti wamelenga kuleta mabadiliko kupitia kauli mbiu maji yanapochafuka ,mwanamke ndiyo huathirika zaidi .mabadiliko yaanze sasa
Amesema kwa sasa Kupitia ufadhili wa shirika la Africa Climate Change Justice Movement (ACCJM) na Global Fund For Women wamekuwa na miradi ambao una unga mkono utekelezaji wa Dira ya Taifa maendeleo ya Tanzania 2050
Kwa kuchangia katika ulinzi wa mazingira, usimamizi endelevu wa rasilimali za maji na ushiriki wa Wanawake katika maendeleo na jamii yenye ustamilivu dhidi ya athali za mabadiliko ya tabia nchi .
Ambapo katika mradi huo tumepanga kuwafikia wanawake ili waweze kuingia kwenye kamati za mazingira kuanzia ngazi ya Mtaa, Kata, Tarafa, hadi Wilaya ili waweze kupaza sauti zao, kuhusu athari za maji machafu kwa mazingira, na afya.









