Na Heri Shaaban, JamhuriMedia, Dar es Salaam
BARAZA Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA) imetangaza sikukuu ya Idd ell adh haa mwaka huu kwa mujibu wa Kalenda ya Kislaam itakuwa Mei 27 mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam Katibu Mkuu wa Baraza la Waislam Tanzania BAKWATA Al haji Nuhu Jabiri Mruma amesema kuwa Sikukuu ya Idd mwaka huu itasaliwa Kitaifa Mkoa Dar es Salaam Mei 27 Siku ya Jumatano katika Msikiti wa Mfalume Mohamed 1V Makao Makuu ya BAKWATA wilayani Kinondoni.
KATIBU wa Baraza Kuu la Waislam Tanzania BAKWATA Al haj Nuhu Jabiri Mruma amesema swala ya Idd siku hiyo itasaliwa saa 1.30 asubuhi na kufuatiwa na Baraza la Idd mara tu baada ya Swala..
Aidha amesema kwa niaba ya Mufti wa Tanzania Shekhe Dkt.Abubakari Bin Zuberi Bin Ally Mbwana aliwatakia Waislam wote Tanzania maandalizi mema ya siku ya Idd.

