Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania-TMA, imewataka wananchi kuchukua tahadhari kuanzia kufuatia kuwepo kwa matarajio ya upepo mkali wa kilomita 40 kwa saa katika mikoa mitano nchini.

Mikoa hiyo ni Dar es Salaam, Pwani, Tanga, Lindi, Mtwara na visiwa vya Unguja na Pemba, hali inayotarajiwa kuwa mbaya kwa siku tano kuanzia leo.

Kwa mujibu wa TMA, hali ya upepo mkali inatarajiwa kuanzia leo kwa baadhi ya maeneo ya ukanda wa Pwani ya Kaskazini mwa Bahari ya Hindi.

Athari zinazoweza kujitokeza kutokana na hali hiyo ni kuathirika kwa baadhi ya shughuli za kiuchumi, uvuvi na usafirishaji baharini.

Kesho, Alhamisi, angalizo limetolewa la upepo wa kilomita 40 kwa saa kwa baadhi ya maeneo ya ukanda wa Pwani ya Kaskazini mwa Bahari ya Hindi katika mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani ikijumuisha visiwa vya Mafia, pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba vilivyopo Zanzibar