
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe Albert Chalamila amefurahishwa na kupongeza Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kwa kuandaa Viwango Marathon kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya kuanzishwa kwa Shirika hilo pamoja na kuendelea kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kuzingatia viwango.
Aidha RC Chalamila amesema mbio hizo ni njia sahihi ya kufikisha elimu kwa jamii kwa namna rahisi, yenye kuvutia na inayogusa maisha ya kila siku ya wananchi hususani Mkoa wa Dar es Salaam.
Viwango Marathon imefanyika mapema leo Mei 23, 2026 katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam ikiwa ni moja ya matukio yanayolenga kuishirikisha jamii katika maadhimisho ya miaka 50 ya TBS.








