Tarehe 3/6/2026 Mahakama ya Wilaya ya Hanang katika shauri la uhujumu uchumi (ECC. No. 7732/2026) imemtia hatiani mshtakiwa Sensa Gidang’ adi Machakwa la matumizi mabaya ya madaraka k/f cha 31 cha PCCA Cap 329 R: E 2023 vikisomwa pamoja na aya ya 21 katika jedwali la kwanza na k/f cha 57(1) na 60(2) vya Sheria ya Kudhibiti Uhujumu uchumi na Makosa ya Kupanga Sura 200 R: E 2023
Mshtakiwa alitumia madaraka yake vibaya kwa kutowasilisha benki kiasi cha TZS. 800,000/= fedha zilizopatikana kutokana na ukodishaji wa shamba la kijiji za na kuzitumia kwa manufaa yake binafsi.
Akisoma hukumu hiyo Mh. Ponella Illoni Hakimu Mkazi Mwandamizi Wilaya ya Hanang’ amemtia hatiani mshtakiwa baada ya mshtakiwa huyo kufanya makubaliano (plea bargaining agreement) na ofisi ya Mkurugenzi wa mashtaka (DPP).
Mshtakiwa amepewa adhabu ya kulipa katika akaunti ya muhanga kiasi cha shilingi milioni moja (TZS. 1,000,000/=) na kuachiliwa kwa masharti ya kutotenda kosa la jinai ndani ya mwaka mmoja.
Hadi hukumu inasomwa mshtakiwa amerejesha kiasi cha Tzs 500,000/= katika akaunti ya kijiji cha Katesh iliyopo Bank ya NMB na kiasi kilichobaki atatakiwa kurejesha kufikia tarehe 25 Juni, 2026 kama ilivyokubaliwa kwenye mkataba wa plea bargaining.


