Mussa Juma, Maipac
[email protected]
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Nurdin Babu amehimiza familia kuandika Wosia ili kupunguza mgogoro kwenye jamii mmoja wa wanandoa hasa mwanaume anapofariki.
Wajane 35 kutoka Mkoa Arusha na Kilimanjaro jana walianza Kampeni ya Kupanda mlima Kilimanjaro na lengo kufikisha kileleni ujumbe wa kuhimiza uandikaji wa Wosia katika familia.
Mkuu huyo wa mkoa akizungumza katika uzinduzi wa Kilimanjaro widows Summit(Kampeni ya Wajane Kupanda mlima Kilimanjaro) Jana mjini Moshi,uliandaliwa na Taasisi ya Wajane Tanzania(TAWIA) Kwa kushirikiana na Serikali na asasi kadhaa za kiraia ikiwepo Taasisi ya Wanahabari ya kusaidia Jamii za pembezoni (MAIPAC)alisema uandishi wa Wosia sio uchoro.
Alisema Wanawake wengi wamekuwa wakipata Shida kubwa baada ya wenza wao kufariki Jambo ambalo sasa linapaswa kupatiwa ufumbuzi.
Mkurugenzi wa TAWIA, Rose sarwatt alisema wameamua katika sehemu ya maadhimisho ya siku ya Wajane Duniani ambaye kilele chake ni June 23 wameanza na Kampeni ya Wajane Kupanda mlima Kilimanjaro.
Alisema baada ya Kupanda mlima Wajane watatembelea hifadhi za Tarangire, Ngorongoro na Serengeti kwenda kuitangaza ujumbe wa kuandika Wosia.
“Baada ya kutoka huko tutakuwa na kongamano mikoani Kilimanjaro ambalo tutashirikisha Zaidi ya Wajane 500 kutoka mikoa mbalimbali nchini.
Awali Rais mstaafu wa chama cha wakili Tanganyika (TLS) Harold Sungusia,alimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro kitabu Maalum ya mwongozo wa Uandishi wa Wosia.
Akizungumza baada ya kukabidhi kitabu hicho alisema amekiandika baada ya utafiti wa kubaini migogoro ya mirathi nchini.
“Kitabu hiki kitusaidia wanafamilia kuandika Wosia Kwa kuzingatia Sheria na hivyo kuondoka migogoro iliyo ya lazima baada ya mmoja wa wanafamilia kufariki”alisema
Wakili.Sungusia ambaye pia ni Mjumbe wa bodi ya TAWIA alisema Wosia ni Andika la mgawanyo wa vitu ambalo mtu analiacha Duniani baada ya kufariki.
Wajane Jana walikuwa wakiendelea na zoezi la Kupanda mlima ambalo pia limefadhikiwa na Shirika la hifadhi za Taifa(TANAPA) na Kampuni za Utalii za kenzel wildlife Safari na Berick Tanzania Tours.
Baadhi ya ambazo zinawezesha maadhimisho hayo ni shirika la Shirika la Wajane Zanzibar (ZAWIA) Kabisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Kaskazini, Shirika la Maendeleo na Utafiti(CORDS),THRDC, Tanzania Woman Fund Trust, Tree of Hope, CRC, LHRC,Voice of Widows Centre,Naserian Organisation,Centre for Widows ,Children na Centre against Gender based Violence na Taasisi za fedha ikiwepo Azania Bank na nyingine kadhaa.










