Staa wa Tasinia ya uigizaji nchini Tanzania Isaa Joseph maarufu kama mzee Onyango amefariki dunia asubuhi ya leo Juni 11, 2026.

Taarifa hizi zimethibitisha na mtoto wake, Joshua Issa na kusema kuwa baba yake amefariki katika Hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam. Kwa sasa msiba upo nyumbani kwa marehemu, Kawe Mzimuni, jijini Dar es Salaam.

Kwa miaka mingi, jina lake limeendelea kubaki kwenye kumbukumbu za mashabiki wa filamu na maigizo ya Kitanzania. Wengi watamkumbuka kwa uchangamfu wake, uhalisia wa uigizaji wake na mchango wake katika kuwalea na kuwahamasisha wasanii chipukizi.

Tunatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu pamoja na jamii nzima ya wasanii.

Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Amina.