Israel imeshambulia Jumamosi kusini mwa Lebanon, ikiwa ni siku moja baada ya nchi hizo mbili kusaini mpango wa kudumisha usalama uliosimamiwa na Marekani.

Mpango huo unalenga kupunguza mvutano katika eneo la mpakani baada ya miezi kadhaa ya uhasama. Shirika la habari la serikali la Lebanon limesema droni za Israel zimashambulia eneo la Nabatieh al-Fawqa, huku jeshi la Israel likidai kuwa lilimlenga mtu ambaye alikuwa tishio kwa vikosi vyake, bila hata hivyo kutoa maelezo zaidi au ushahidi.

Katika makubaliano hayo, Israel inatakiwa kuwaondoa wanajeshi wake katika maeneo mawili kusini mwa Lebanon ambayo yatatakiwa kudhibitiwa na jeshi la nchi hiyo. Kundi la Hezbollah linaloungwa mkono na Iran halikushiriki na linayapinga makubaliano hayo.