Na Mwandishi wetu,JamhuriMedia,
Dar es Salaam
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam limekanusha taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zikidai kuwa wananchi wamechoma moto gari la polisi katika eneo la Mwenge, likisema taarifa hizo ni za uongo na zinalenga kupotosha umma.
Katika taarifa iliyotolewa leo,Julai 4,2026 Dar es Jeshi la Polisi limesema hakuna gari lake lililochomwa moto kama inavyodaiwa kwenye ujumbe unaosambazwa mtandaoni, na limewataka wananchi kupuuza taarifa hizo ambazo zinaweza kusababisha taharuki isiyo na msingi.
Aidha, Jeshi hilo limesema linaendelea kuchukua hatua za kisheria na kisayansi kuwabaini watu au makundi yanayosambaza taarifa za uzushi ili wakamatwe na kufikishwa kwenye vyombo husika vya sheria.
Jeshi la Polisi limetoa wito kwa wananchi kuhakikisha wanathibitisha taarifa wanazopokea kabla ya kuzisambaza, ili kuepusha upotoshaji wa umma na kulinda amani na utulivu wa nchi.



