Uhispania imetangaza hali ya dharura ya kitaifa mjini Madrid na mkoa wa Avila, karibu na mji mkuu, kufuatia milipuko kadhaa ya moto wa nyika inayoteketea bila kudhibitiwa.

Uhispania imetangaza hali ya dharura ya kitaifa mjini Madrid na mkoa wa Avila, karibu na mji mkuu, kufuatia milipuko kadhaa ya moto wa nyika inayoteketea bila kudhibitiwa.

Hatua hiyo, iliyotangazwa na Wizara ya Mambo ya Ndani, inalenga kuharakisha utoaji wa rasilimali za kukabiliana na moto huo, ambao katika eneo la Madrid pekee umelazimisha watu 10,000 kuhama makazi yao.

Aidha, usimamizi wa operesheni za dharura umewekwa chini ya kikosi cha kijeshi cha kushughulikia majanga.

Kwa ujumla, zaidi ya watu 10,000 wamehamishwa kutoka maeneo mbalimbali ya Madrid katika siku za karibuni, huku mioto kadhaa ya misituni ikiendelea kuwaka kwa wakati mmoja katika eneo hilo.

Karibu hekta 125,000 za ardhi tayari zimeteketea kwa moto nchini humo mwaka huu.