Taarifa ya jeshi la Israel IDF imesema shambulio hilo lilimlenga kamanda wa Hamas, likimtuhumu kwamba alikuwa akipanga mashambulizi dhidi ya vikosi vya Israel vinavyofanya kazi katika ukanda huo.
Israel imefanya shambulio lake la kwanza la anga huko Gaza baada ya muda wa zaidi ya wiki moja. Taarifa ya jeshi la Israel IDF imesema shambulio hilo lilimlenga kamanda wa Hamas, likimtuhumu kwamba alikuwa akipanga mashambulizi dhidi ya vikosi vya Israel vinavyofanya kazi katika ukanda huo.
Hata hivyo, Shirika la ulinzi wa kiraia la Gaza lililo chini ya Hamas limesema shambulio hilo liliwalenga raia waliokuwamo kwenye chombo cha usafiri. Shirika hilo limeongeza kwamba shambulio hilo limemuua mtu aliyefahamika kwa jina la Mohanad Saada na kuwajeruhi watu wengine watano.
Mwezi uliopita, Rais Trump wa Marekani alitangaza kwamba Bodi yake ya Amani ilikuwa imefikia makubaliano ya “kihistoria” na Hamas na makundi mengine ya wanamgambo wa Palestina katika Ukanda wa Gaza ya kupokonya silaha.
Lakini baadaye Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu alitangaza kwamba Israeli imeukataa mpango huo.


