Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Dodoma
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda,Biashara,Kilimo na Mifugo imeipongeza TBS kwa kutekeleza majukumu yake ya udhibiti ubora kwa ufanisi.
Pongezi hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe.Deogratias Mwanyika kwaniaba ya kamati wakati wa kikao cha Kamati cha kupokea taarifa ya utekelezaji wa majukumu,katika, ofisi za Bunge Jijini Dodoma mapema leo.
Mhe.Mwanyika amesema juhudi zinazofanywa na TBS katika kuhakikisha usalama na ubora wa bidhaa zinazotumiwa na Watanzania zinaonekana hata hivyo ametoa rai kwa TBS kuendelea kutoa elimu na kuongeza jitihada sambambana na kuwa na programu maalum za kushughulikia bidhaa zinazoingizwa nchini kwa njia zisizo rasmi.
Naye Mhe. Waziri wa Wizara ya Viwanda na Biashara Mhe. Judith Kapinga(Mb) ameishukuru kamati hiyo na kuahidi kuyafanyia kazi maelekezo na ushauri uliotolewa na kamati hiyo ili kuendelea kurahisisha utendaji kazi wa TBS.
Vile vile Mhe.Kapinga amesema lengo la Wizara kupitia TBS ni kuhakikisha kunakuwa na bidhaa zenye ubora na usalama katika soko zinazozalishwa ndani na zinazotoka nje ya nchi.








