Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Hamza S. Johari, amekutana na Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Bw. Andrew Lentz, na ujumbe wake kwa ajili ya kufanya mazungumzo kuhusu masuala mbalimbali yenye lengo la kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Marekani.

Kikao hicho kimefanyika tarehe 20 Agosti, 2026 katika Ofisi Ndogo ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jijini Dar es Salaam, ambapo katika mazungumzo hayo, wamejikita katika masuala mbalimbali ya maendeleo, mipango ya kimkakati ya Uwekezaji, pamoja na maeneo mengine ya ushirikiano wa pande mbili.

Pande zote mbili zimesisitiza umuhimu wa kuendeleza mazungumzo, ushirikiano wa kisheria na kitaalamu, pamoja na diplomasia endelevu katika kusukuma mbele vipaumbele vya pamoja na kukuza ubia wenye manufaa kwa Tanzania na Marekani.