Rais Samia kuzindua rasmi kituo cha kuzalisha umeme cha JNHPP Agosti 22
Uzinduzi huo unaashiria hatua kubwa katika safari ya Tanzania ya kuimarisha upatikanaji wa umeme wa uhakika, kuchochea shughuli za uzalishaji na kuimarisha uchumi wa Taifa.
Tayari mitambo yote tisa yenye uwezo wa kuzalisha Jumla ya Megawati 2,115 imekamilika na kuingizwa katika Gridi ya Taifa.
Mradi huo umekamilika kwa gharama za takribani Sh. Trilioni 7.5 zilizofadhiliwa asilimia 100 na Serikali ya Tanzania.






