Na Francisco Peter, JamhuriMedia, Dar es Salaam
Mbunge wa Kigoma Mjini, Mhe. Clayton Revocatus Chipando maarufu ka Baba Revo ameingia makubaliano ya kutiliana saini na Mfuko wa Uwekezaji uitwao Zan Securities ambao umetajwa kuja kutoa fursa kwa Watanzania.
Akizungumza Jijini Dar es Salaam leo Agosti 25, 2026 amesema kwa kuanza kwa utumiaji wa mfuko huo ili mwananchi aanze kupata gawio atatakiwa kuanza na uwekezaji kuanzia sh. 20,000
” Napenda kuwapa taarifa Watanzania kuwa mifuko ya namna hii inaepusha mlolongo wa matatizo yanayotajwa kuwepo mitaani ya kuchangishana fedha na kuziweka kwa watu wanaoitwa vijumbe,”amesema Baba Revo.
Amesema mfuko huo alioingia nao mkataba utatoa malengo juu ya fursa chanya kwani zipo faida nyingi ambapo , mteja anayejiunga atachagua kuwekeza katika mifuko atakaokuwa amechagua.
Tayari wamefanya mifumo ya kushiriki katika uwekezaji kwa kutumia simu aina ya Smart Phones ambapo kwa maelekezo mteja anaweza kupiga 0750011250 katika kupata njia yenye maelekezo rahisi ya kujiunga na fursa za uwekezaji.
Ndiyo, Zan Securities Limited walifanya uzinduzi wa mifuko yao mipya ya uwekezaji katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.
ZAN Timiza ETF inatofautiana na mifuko mingine ya uwekezaji kwa kuwa vipande vya mfuko huo vitauzwa na kununuliwa kupitia Soko la Hisa la Dar es Salaam.
Kampuni inayo mshauri juu ya uwekezaji Fadhila Mbura pamoja na Isaac Lubeja ambaye ni Mkuu wa Ushauri kampuni hiyo walihusika katika utiaji wa saini ambapo jamii imekumbushwa kuwa uwekezaji si kwa ajili ya makundi maalum bali ni kwa mtu yoyote anayewekeza kwenye masoko ya dhamana.
Ambapo viongozo hao kwa psmoja wamesema kuwa Kampuni ya ZAN Securities, tayari ina mifuko yake mipya ya uwekezaji ya ZanTimiza ETF na Timiza Fund Plus.
Lengo kuu la mifuko hiyo imeelezwa kuwa ni kufungua fursa mpya na za kisasa za kiuwekezaji pamoja na kutoa jukwaa kwa wananchi na wawekezaji kukutana na kubadilishana mawazo na wataalamu wa sekta ya fedha na masoko ya mitaji.
ZAN Securities inawakaribisha wananchi na wawekezaji wote ili kushiriki katika uzinduzi huu. Kwa maelezo zaidi na usajili, wasiliana nao kupitia namba ya simu +255 750 011 250 au tembelea tovuti yao ya www.zansec.co.tz.



