Na Aziza Nangwa, JamhuriMedia, Dar es Salaam

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amewataka wadau wa
mnyororo wa uchukuzi na usafirishaji mizigo ,kushirikiana kutafuta suluhisho la muda mrefu la changamoto zinazoikabili sekta hiyo, ikiwamo foleni za malori, ukosefu wa maeneo maalumu ya maegesho na msongamano wa magari katika jiji

Chalamila ameyasema hayo wakati wa akiongoza kikao cha wadau wa mnyororo wa usafirishaji,kilichofanyika katika ukumbi wa Idd Nyundo Manispaa ya Temeke

Kikao hicho kiliwakutanisha,
viongozi mbalimbali na vua ulinzi na usalama kujadili mikakati ya kudhibiti msongamano wa malori na foleni

Katika kikao hicho wadau walipata nafasi
ya kutoa maoni yao juu ya kuboresha mazingira ya usafarishaji na
kupunguza msongamano wa Maroli katika maeneo mbalimbali

Chalamila amesema lengo la kikao hicho ni kupata majawabu ya pamoja ya muda mrefu badala ya kila mdau kushughulikia changamoto kwa upande wake.

Amesema baada ya kukutana na wadau wa usafirishaji Dar es Salaam, miongoni wa hoja ni kupanua wigo mpaka mkoa wa Pwani pamoja na mikoa mingine inayohusika katika mnyororo wa usafirishaji wa mizigo kutoka na kwenda Bandari ya Dar es Salaam.

“Tunapozungumzia Pwani tunatanua wigo. Tutamshirikisha Waziri wetu wa
TAMISEMI ili aweze kuwa na kikao kikubwa na wakuu wa mikoa na wadau wa
namna hii, kwa sababu wote tunahusika,” amrsema

Amesema changamoto za usafirishaji haziishii Dar es Salaam pekee, bali zinaunganisha mikoa mbalimbali ikiwamo Tanga, Morogoro, Mbeya na
Songwe, hasa katika njia zinazotumika kusafirisha mizigo kwenda maeneo
ya mipakani.

Amesema moja ya hoja zilizojitokeza katika kikao hicho ni ukosefu wa eneo maalumu la malori, wakati maeneo mengi yaliyopo yameelekezwa zaidi kwa mabasi.

Amesema suala hilo linahitaji kuangaliwa na wakurugenzi pamoja na wataalamu wa mipango miji ili kupata eneo linalofaa kwa ajili ya malori na upunguzamsongamano katika maeneo ya mijini.

Chalamila pia alizungumzia umuhimu wa kupanga matumizi ya maeneo
yanayozunguka Bandari ya Dar es Salaam ili shughuli zinazofanyika
katika maeneo hayo ziendane na mahitaji ya bandari.

Amesema iwapo maeneo yaliyo karibu na bandari yatatumika kwa shughuli
zisizohusiana na bandari, hali hiyo inaweza kuongeza msongamano na
usumbufu kwa wananchi, madereva wa malori na wadau wengine wa usafirishaji.

“Unapokuwa na bandari jirani yako, inapaswa kuwa inafanya shughuli za
bandari.

Kama hakuna mipango hiyo, kila mtu atakuwa analia; mwananchi analia, wenye malori wanalalamika na hata Mkuu wa Mkoa analalamika,”
amesema

.
Mwakilishi kutoka Chama cha Mawakala wa Mipaka na Usafirishaji Mizigo
Tanzania Ernest Lobulu ameiomba Serikali kuongeza maeneo ya kuhudumia
malori na kutumia maeneo ya hifadhi ya barabara

Amesema malori yana umuhimu mkubwa katika uchumi wa nchi kwa kuwa ndiyo yanayosafirisha mizigo kutoka bandarini kwenda maeneo mbalimbali, linatakiwa kupatiwa maeneo maalum yatumike kama dharula wakati serikali inasubiria suluhisho la kudumu.

Lobulo amesema licha ya baadhi ya wasafirishaji kuiona kama kero, ina
umuhimu katika kuhakikisha mizigo inapimwa kabla ya magari kuendelea
nasafari,kinacho hitajika na uboreshaji wa utaratibu

Amesema ni muhimu magodauni nje ya maeneo yenye msongamano mkubwa wa watu badala ya kuyaweka katikati ya jiji, kwa kuwa uwepo wa magodauni katikati ya mji huvutia malori na magari mengi kuingia katika maeneo
yenye msongamano.

Amesema wafanyabiashara wanapaswa kutumia maeneo yao ya biashara na kuacha barabara za umma wazi kwa matumizi ya wananchi na usafirishaji.

Mwenyekiti wa Chama cha wamiliki wa Maroli Chuki Shabani alipendekeza Serikali itumie eneo la Kibaha,
Misugusugu, kwa ajili ya kuanzisha kituo kikubwa cha malori kwa kuweka huduma muhimu.

Aidha, alipendekeza Serikali ipitie upya maeneo yote ya bandari kavu
(ICD) yaliyopo nchini ili kubainika kama hayana uwezo wa kuhudumia malori kwa ufanisi yachukuliwe hatua.