*Familia yakubali maziko baada ya mvutano mrefu

*Baba amwachia Mungu huku akitaka haki itendeke

*Ripoti za hospitali zaacha maswali kuhusu majeraha

Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Bukoba

Baada ya mvutano wa muda mrefu kati ya familia ya Frank Stanley na Jeshi la Polisi mkoani Kagera kuhusu mazingira ya kifo chake, kijana huyo amezikwa jana katika Kijiji cha Karonge, Bukoba mkoani Kagera, huku maswali kuhusu kilichompata yakiendelea kusubiri majibu.

Maziko yaliyohudhuriwa na mamia ya wananchi yamefanyika baada ya familia kukubali kuuchukua mwili uliokuwa umehifadhiwa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando, Mwanza. Awali, familia ilitaka ufafanuzi kuhusu majeraha aliyokuwa nayo Frank kabla ya kufariki dunia.

Baba mzazi, Stanley Ndibalema, amesema uamuzi huo umefikiwa baada ya vikao kadhaa na viongozi wa Polisi pamoja na kupitia taarifa za kitabibu kutoka hospitali za Bukoba na Bugando. Amesisitiza kuwa kumzika mwanawe hakumaanishi kuacha kudai ukweli na haki.

“Nimesikia mengi sana juu ya mwanangu Frank, hakuwahi kuugua ugonjwa wa kisukari wala figo. Amefika mikononi mwa Polisi ndiyo yakatokea yote haya, namwachia Mungu jambo hili. Inauma mno kukatisha ndoto za kijana mdogo hivi,” amesema Ndibalema.

Frank alifariki dunia Septemba 2, mwaka huu, akiwa anapatiwa matibabu Bugando, baada ya kuwa chini ya ulinzi wa Polisi mkoani Kagera. Familia inadai alichukuliwa akiwa mzima, lakini baadaye ikapata taarifa kwamba amelazwa hospitalini akiwa katika hali mbaya. Kwa familia, kilichokuwa kinazua mvutano si taratibu za maziko pekee, bali pia namna ya kupata taarifa zinazoweza kueleza kilichotokea kabla ya Frank kupelekwa hospitalini. Ndiyo

KWA HABARI ZAIDI SOMA GAZETI LA JAMHURI LA OKTOBA 13- 19, 20206