Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Dar es Salaam
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda, amesema Serikali inalenga kuona ubunifu unaofanywa na Watanzania unavuka hatua ya majaribio na kuanza kuzalisha bidhaa zinazoweza kuuzwa sokoni, ili kuchochea maendeleo ya teknolojia na kupunguza utegemezi wa bidhaa kutoka nje ya nchi.
Profesa Mkenda amesema hayo leo Novemba 11,2026,Jijini Dar es salaam wabunifu wanapaswa kuanza na teknolojia ndogo na bidhaa rahisi zinazoweza kuzalishwa nchini, kama vipuri vya pikipiki ambavyo kwa sasa vinaagizwa kutoka nje, kisha kuongeza uwezo hatua kwa hatua hadi kufikia uzalishaji wa bidhaa kubwa zaidi.
Amesema si lazima kuanza kwa kutengeneza bidhaa kubwa kama magari au helikopta, bali ni muhimu kujenga uwezo kwa kuanza kuzalisha sehemu za bidhaa hizo na baadaye kuongeza kiwango cha uzalishaji kadiri teknolojia na uwezo unavyokua.
Akitolea mfano wa ubunifu uliofanywa na mwanasayansi aliyefanya masomo ya PhD katika Chuo Kikuu cha Nelson Mandela African Institute of Science and Technology, Arusha, amesema amebuni teknolojia ya kutengeneza sementi kwa kuchanganya pozolana, inayolenga kupunguza gharama za uzalishaji, matumizi ya nishati na kuongeza uimara wa sementi. Amesema tayari mazungumzo yanafanyika na kampuni za uzalishaji wa sementi ili ubunifu huo ufikishwe sokoni.
Hata hivyo watafiti na vyuo vikuu nchini kuongeza juhudi za kufanya tafiti za kisayansi kuhusu mimea inayotumika kama dawa za asili, ili kubaini ufanisi wake katika kutibu magonjwa mbalimbali, kiwango sahihi cha matumizi pamoja na madhara yanayoweza kujitokeza.
Hatua hiyo inalenga kuhakikisha kuwa matumizi ya mimea tiba yanazingatia ushahidi wa kisayansi badala ya kutegemea imani na maelezo yasiyothibitishwa kuhusu uwezo wake wa kutibu magonjwa.
Prof Mkenda akizungumzia kuhusu umuhimu wa matumizi ya sayansi, teknolojia na ubunifu katika sekta ya tiba, mmoja wa viongozi wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) alisema tafiti nyingi kuhusu mimea inayodaiwa kuwa na uwezo wa kutibu magonjwa zimekuwa zikifanyika nje ya nchi, huku taarifa zake zikipelekwa kwa watafiti wa mataifa mengine kwa ajili ya uchambuzi.
Waziri kizungumza kuhusu umuhimu wa matumizi ya sayansi, teknolojia na ubunifu katika sekta ya tiba, mmoja wa viongozi wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) alisema tafiti nyingi kuhusu mimea inayodaiwa kuwa na uwezo wa kutibu magonjwa zimekuwa zikifanyika nje ya nchi, huku taarifa zake zikipelekwa kwa watafiti wa mataifa mengine kwa ajili ya uchambuzi.
Alisema ni wakati sasa Tanzania kutumia wataalamu wake wa vyuo vikuu na taasisi za utafiti kufanya uchunguzi huo ndani ya nchi, ili kubaini kwa uhakika mimea ipi ina uwezo wa kutibu, inatibu kwa kiwango gani na kama ina madhara kwa watumiaji.
“Tunataka mimea hiyo ifanyiwe utafiti hapa nchini na sisi tuamue tujue kama kweli inaweza kutibu, inatibu kiasi gani na kama kuna madhara, ni namna gani ya kuzuia madhara hayo. Tungependa sayansi itumike ili tusifanye masuala ya tiba kama ramli,” alisema.
Alifafanua kuwa hatua muhimu katika kuthibitisha usalama na ufanisi wa dawa ni kufanya utafiti wa awali unaojulikana kama Pre-clinical Trial, unaohusisha majaribio ya kisayansi kwa kutumia wanyama kabla ya dawa husika kuanza kufanyiwa majaribio kwa binadamu.
Amesema utafiti huo husaidia kubaini kama dawa ina dalili za kutibu ugonjwa husika na kama inaweza kusababisha madhara makubwa kabla ya kuingia katika hatua ya Clinical Trial, ambayo huhusisha majaribio kwa binadamu.
Aidha kutakiwa na maadhimisho ya miaka 40 ya COSTECH yanalenga kuhamasisha matumizi ya sayansi, teknolojia na ubunifu katika sekta mbalimbali, yakianzia na kaulimbiu ya kuendeleza sayansi katika sekta ya tiba (Advancing Science in Medical Field), kabla ya kuendeleza ajenda hiyo katika kilimo, uvuvi na maeneo mengine.
Alieleza kuwa kilele cha maadhimisho hayo kitafanyika Novemba 17 na 18, ambapo maonesho ya sayansi, teknolojia na ubunifu yataanza Novemba 17 katika Kituo cha Mlimani City jijini Dar es Salaam na kuendelea Novemba 18, huku Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba akitarajiwa kuhudhuria na kuhitimisha maadhimisho hayo.
Watanzania, wadau wa sayansi, watafiti na waandishi wa habari kujitokeza katika maonesho hayo ili kujionea kazi zilizofanywa na COSTECH pamoja na ubunifu mbalimbali unaoendelea nchini.


