Thamani ya mikopo endelevu ya Benki ya NMB imeongezeka kwa asilimia 28.3 na kufikia Sh608 bilioni mwaka 2025, ikichangia uwekezaji katika miradi inayolenga kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, kukuza uchumi na kuboresha maisha ya wananchi.
Mafanikio hayo yamebainishwa katika Ripoti ya Uendelevu ya NMB ya mwaka 2025, iliyozinduliwa jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Dkt. Richard Stanslaus Muyungi.
Kati ya fedha hizo, Sh328 bilioni zilielekezwa katika miradi inayochangia utunzaji wa mazingira, ikiwemo nishati safi na kilimo kinachohimili mabadiliko ya tabianchi, huku Sh280 bilioni zikielekezwa katika miradi yenye manufaa ya kijamii na kiuchumi. Aidha, benki hiyo ilipunguza uzalishaji wa gesi chafuzi unaotokana na shughuli zake kwa asilimia 7.3 na kupanda miti milioni 1.4 mwaka 2025.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi na Afisa Mkuu wa Fedha wa NMB, Juma Kimori, alisema uendelevu ni msingi wa mkakati wa benki hiyo katika utoaji wa mikopo, uwekezaji na kuchangia maendeleo ya Tanzania. Tangu mwaka 2022, NMB imekusanya Sh621 bilioni kwa ajili ya ufadhili endelevu, ikiwemo Sh147 bilioni kupitia Hati Fungani ya Uendelevu ya Jamii mwaka 2025.
Uzinduzi huo uliambatana na warsha ya uendelevu iliyoandaliwa na NMB kwa kushirikiana na FMO na Finance in Motion, iliyowakutanisha wawakilishi wa Serikali, taasisi za fedha na wadau wa maendeleo kujadili namna ya kuongeza uwekezaji katika miradi endelevu, kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kupanua fursa za kiuchumi kwa wananchi.
Pakua Ripoti kamili ya Uendelevu ya NMB ya mwaka 2025 kupitia kiungo kifuatacho:









