Na Manka Damian , JamhuriMedia ,Mbeya

CHAMA cha Kutetea Haki na Maslahi ya Walimu Tanzania (CHAKAMWATA), kimempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kupandisha mshahara kwa watumishi wa umma kwani ameweka historia kwa nchi na
haijawahi kutokea kwani Rais amegusa maisha ya Watanzania walio wengi.

Kauli hiyo imetolewa Mei 5, 2025 na Katibu Mkuu CHAKAMWATA, Meshack Kapange wakati akizungumza na waandishi wa habari Makao makuu ya chama hicho yaliyopo eneo la Mafiati Jijini Mbeya kuhusiana na maadhimisho ya siku ya wafanyakazi ambayo kitaifa ilifanyika mkoani Singinda.

Aidha Kapange amesema kuwa Rais Dkt .Samia kupandisha kiwango cha mshahara kwa watumishi kimeleta faraja kubwa kwa ongozeko hilo.

“Sisi wafanyakazi ni mikono ya watanzania wengine ya kuchumia fedha hatuli fedha kama fedha tunakula mahindi, matembele, bamia ndo vyakula vyetu, tukilipwa vibaya tunakwenda kwa watanzania wenzetu maskini kwenda kununua vitu vibaya,tukilipwa vizuri tunakwenda kununua vizur unamkuta Bibi hajui nguo alifua lini bado unabembeleza bado akupunguzie”amesema Katibu Mkuu huyo .

Aidha Kapange amesema kuwa kwa mtumishi akilipwa vizuri hawezi kuwa na maisha duni ya kuomba ,hivyo kubadilisha mshahara kwa wafanyakazi kutabadili maisha kwa jamii na Taifa kwa ujumla .

Akizungumzia kuhusu kauli ya TUCTA ya kumuomba Rais Samia kuruhusu kubadilisha sheria uhuru wa vyama vya wafanyakazi hauanzii kwenye sheria bali unaanzia kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais Samia ni binadamu angekosa tu hekima na kujibu hebu shughulikieni hilo tayari ilikuwa ni taflani kwenye nchi hii tungelaumu Rais kuwa Rais amevunja katiba lakini angekuwa amesabishwa na watu hawa

“Tumeona tusikae kimnya tutoke hadharini kuwaambia TUCTA na wanachama wake kuwa kitendo cha kutaka kumpotosha Mh Rais kumtaka kutoa maelekezo ya kuvunja katiba ya nchi ambayo ameapa kuilinda “amesema Katibu Mkuu huyo.

Mmoja wa walimu ambaye hakutaka jina lake kuandikwa amesema kuwa kitendo cha kuongezeka kwa mshahara kimewapa faraja sana watumishi wa umma .

“Rais Samia amejua kutukosha kwa ongezeko la mshahara kiukweli hasa sisi walimu tumepata faraja kubwa kwani haijawahi kutokea hivyo ongozeko hili limetupa ari ya kufanya kazi zaidi kwa kujituma “amesema .

Katibu Mkuu wa Chama cha Kutetea Haki na Maslahi ya Walimu Tanzania, Meshack Kapange