JamhuriComments Off on Rais Mwinyi awaaga Mahujaji watarajiwa Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Katibu Mtendaji Kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana Zanzibar Sheikh Abdalla Talib, alipowasili katika viwanja vya Masjid Jamiu Zinjibar, kwa ajili ya kuwaaga Mahujaji Watarajiwa wa Zanzibar na (kushoto kwake) Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Hassan Othman Ngwali, hafla hiyo iliyofanyika leo 17-5-2025.(Picha na IkuluMAHUJAJI Watarajiwa wa Zanzibar wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) wakati akizungumza na kuwaaga, hafla hiyo iliyofanyika katika Masjid Jamiu Zinjibar Mazizini Wilaya ya Magharibi “B” Unguja leo 17-5-2025.(Picha na Ikulu)RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na kutowa nasaha zake, wakati wa Semina ya kuwaaga Mahujaji Watarajiwa wa Zanzibar wanaotarajiwa kuondoka mwezi huu kuelekea Saudi Arabia kwa ajili ya Hijja, iliyofanyika katika Masjid Jamiu Zinjibar Mazizini Wilaya ya Magharibi “B” Unguja leo 17-5-2025.(Picha na Ikulu)RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Mahujaji Wataraji katika kuitikia dua ikisomwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh. Saleh Omar Kabi, wakati wa Semina ya Kuwaaga Mahujaji Watarajiwa wa Zanzibar, wanaoelekea Nchini Saudi Arabia kwa ajii ya Hijja, hafla hiyo iliyofanyika katika Masjid Jamiu Zinjibar Mazizini Wilaya ya Magharibi “B” Unguja.(Picha na Ikulu)