Na Lookman Miraji

Mashindano ya taifa kwa vijana katika mchezo wa kuogelea yameendelea kuleta msisimko kwa wadau wa mchezo huo nchini. Mashindano ya hayo ya taifa kwa vijana yamefanyika mwaka huu ikiwa ni sehemu ya kalenda ya mwaka ya chama cha kuogelea nchini(TSA).

Tofauti na ilivyozoeleka mara zote ,mara hii mashindano hayo yamehusisha vijana wenye umri chini ya miaka 12 kutoka vilabu mbalimbali vya kuogelea kutoka ndani na nnje ya nchi.

Wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi, Akizungumza Afisa wa michezo kutoka baraza la taifa la michezo (BMT), Ndg: Charles Maguzu amesema kuwa serikali inaendelea kuunga mkono jitihada zinazofanywa na mashirikisho ya michezo nchini katika kukuza ustawi wa michezo.

Aidha Afisa Maguzu ameongeza pia katika suala zima la ukarabati miundombinu ya michezo serikali inaendelea na ukarabati mkubwa wa mabwawa ya kuogelea na pindi mchakato huo utakapokamilika utakuja kupunguza baadhi ya changamoto katika michezo.

Mwenyekiti wa chama cha mchezo wa kuogelea nchini, Ndg:David Mwasyoge nae ameongeza kuwa mashindano hayo ni maalum kwa vijana wadogo kwenye mchezo huo ambao dhamira yao kama viongozi ni kuandaa vipaji vipya katika mchezo kwaajili ya siku zijazo.

Kwa mwaka huu mashindano hayo yamejumuisha jumla ya vilabu 18 vya kuogelea na waogeleaji vijana zaidi ya 200.

Mashindano hayo yamefanyika kuwa ya siku mbili jijini ambapo yalianza Jumamosi ya Juni 14 na kuhitimishwa kwake jumapili ya jana Juni 15 , 2025.