Na Mwandishi Wetu, Tanga
Mwenge wa Uhuru umezindua mradi wa mita za maji za malipo ya kabla (LUMAKU) wenye thamani ya Sh bilioni 1.8 ambao ni utekelezaji wa agizo la Rais Samia la kupunguza malalamiko ya ankara kubwa za maji kutoka kwa wananchi.
Mradi huo ambao unatekelezwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jiji la Tanga, (Tanga UWASA wenye gharama ya Sh bilioni 1.8 mpaka sasa umeweza kuwafikia wateja zaidi ya 2,000.
Akizungumza wakati Mwenge wa Uhuru ulipofika kufanya ufunguzi wa mradi huo Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa, Ismail Ali ussi amesema kuwa mfumo huo unakwenda kuwasaidia wananchi na unakwenda kupunguza malalamiko kutoka Kwa wateja.
Nawapongeza Tanga Uwasa kwa kutekeleza agizo la Rais Samia la kuja na suluhisho la malalamiko ya ankara za maji kutoka kwa wananchi kwani kupitia mita hizi sasa hakuna mwananchi ambaye ataweza kuonewa kwani anatumia alicholipi,”alisema kiongozi huyo.
Hata hivyo, meneja mradi wa kufunga meta za malipo ya kabla Alawi Ahmad amesema kuwa kwa awamu ya kwanza mradi huo umelenga kufunga meta 4,000 lakini mpaka sasa wamefunga mita 2020 sawa na asilimia 51% ya malengo ya mradi,”amesema Ahmad.

