Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu Prof. Daniel Mushi, wakati alipowasili katika Kongamano la Kumi na Tatu la Kisayansi la Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili, kwenye Kampasi ya Mloganzila (MUHAS) jijini Dar es Salaam, Juni 18, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akifafanuliwa jambo na Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali, Dkt. Said Kilindimo, katika Kongamano la Kumi na Tatu la Kisayansi la Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili, Kampasi ya Mloganzila (MUHAS) jijini Dar es Salaam, Juni 18, 2025.  Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu Prof. Daniel Mushi na kulia ni Makamu Mkuu wa Chuo hicho Profesa Appolinary Kamuhabwa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza, kwenye Kongamano la Kumi na Tatu la Kisayansi la Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili, kwenye Kampasi ya Mloganzila (MUHAS) jijini Dar es Salaam, ambalo alikua Mgeni rasmi Juni 18, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akikabidhiwa Tuzo na Naibu Katibu Mkuu Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu Prof. Daniel Mushi, iliyotolea na Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili ya kutambua mchango wake katika ukuaji wa mafunzo, tafiti na bunifu nchini, kwenye Kongamano la Kumi na Tatu la Kisayansi la Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili, Kampasi ya Mloganzila (MUHAS) jijini Dar es Salaam, ambalo alikua Mgeni rasmi Juni 18, 2025. Kulia ni Makamu Mkuu wa Chuo hicho Profesa Appolinary Kamuhabwa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)