Na Magrethy Katengu, JamhuriMedia, Dar es Salaam

Chama cha ACT Wazalendo kimetangaza kujitoa kwenye Serikali ya Umoja wa Kitaifa kutokana na kutotekelezewa hoja zao tatu ikiwemo fidia kwa waliopata madhara katika uchaguzi 2020, kuundwa Tume ya Kijaji kuchunguza uvunjifu wa haki za binadamu kwenye uchaguzi Mkuu 2020 na Mageuzi katika mfumo wa uchaguzi.

Ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam Macho 8,2024 Katibu Mkuu wa cha hicho Ado Shaibu ambapo amebainisha kuwa uamuzi huo ulifikiwa na Kikao cha Halmashauri kuu Taifa ya chama cha ACT Wazalendo kilichofanyika Machi 4, 2024 na kutoa agizo kwa Kamati ya Uongozi Taifa kukutana na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassani na Rais wa Zanzibar Hussein Mwinyi kupata muafaka wa hoja zao .

“ACT Wazalendo kujitoa kwenye Umoja wa Kitaifa sababu kutotekelezewa makubaliano yaliyoingiwa na Marehemu Maalim Seif Hamadi kwa niaba ya chama hiko na Rais Hussein Mwinyi kabla ya ACT Wazalendo kujiunga na Serikali ya Umoja wa Kitaifa kwani kati ya hoja zao hakuna hata moja lililotekelezwa na tumekaa kimya kwa muda sasa tumechoka sasa tumeamua kufanya uamuzi huu” amesema Katibu Mkuu

Katika hatua nyingine chama hicho kilikaa Machi 7, 2024 na kufanya uteuzi Katibu Mkuu na Manaibu katibu Mkuu na Halmashauri Kuu iliidhinisha Ado Shaibu kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo kwa kipindi kingine cha miaka mitano

Aidha naye Mwenyekiti wa Mpya wa Chama cha ACT Wazalendo, Othmani Massoud Othmani kwa Mamlaka.aliyonayo amefanya uteuzi wa Wajumbe wa Halmashauri kuu ya chama Marry Zakaria na Nani Kadika pia Naibu Mwanasheria Mkuu wa Chama Bonifasia Matunda, Katika idara ya habari Uenezi na Mahusiano ya Umma Katibu Salim Abdalah Biman Naibu wake Shangwe Mika Ayo na Idara ya Fedha Racher Kimambo na Hafidh Abdulrahmani

By Jamhuri