Na Magrethy Katengu, JamhuriaMedia, Dar es Salaam

Chama cha Act -Wazalendo kimesema kitahakikisha kinafuatilia miswada waliyopeleka bungeni hadi ipitishwe kuwa sheria ikiwemo kudai tume huru ya uchaguzi aliyepoteza kadi ya kura au kufutika alipie fedha apewe nyingine, Tume ya Uchaguzi iwe na jukumu la kusimamia chaguzi zote kuanzia Serikali za Mtaa hadi udiwani, ubunge hadi urais.

Ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe katika mkutano mkuu wa Halmashauri Kuu ya Taifa chama hicho ambapo wamesema wamepeleka mapendekezo 10 bungeni na mapendekezo sita ndiyo yaliyopita ili kusaidia kusukuma mbele mageuzi ya demokrasia wakati Taifa linaelekea katika uchaguzi wa viongozi mbalimbali .

“Ndugu wajumbe wa Halamashauri kuu miswada ilikuwa na mambo mengi sana na chama chetu kupitia kamati kuu yetu tulitambua na kupendekeza mambo 10 na mambo sita yalipitishwa na yalichukuliwa kama yalivyo na kuwekwa katika sheria hizo mpya na baadhi ya mambo hayakukubaliwa ni jambo la kawaida katika majadiliano yoyote tungeshangaa kama tungepata 10” amesema Zitto.

Sambamba na hayo amesema mabadiliko ni mchakato siyo tukio la siku moja siku zote maneno ya Hayati Rais Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyoyatoa akiwa Tabora mwaka 1958 kwamba ” Ni busara ikiwa mtu mmoja amedai kiasi fulani kwa mdeni wake akilipa sehemu fulani ya kiasi anachodaiwa inafaa kipokelewe kiasi hicho na palepale.iendelee kudaiwa sehemu iliyobaki” hivyo tujipe moyo basi mabadiliko ni hatua muhimu sana katika safari hiyo ya kuelekea uchaguzi.

Sanjari na hayo amewasisitiza kuwa na uongozi wa pamoja kwani jambo kubwa kujenga utamaduni wa viongozi wote kukaa kwa pamoja kujadili na kufanya maamuzi ya pamoja kwa chama kilipotoka mshikamano ndiyo umewezesha chama kuimarika hivyo kama wewe umepewa dhama na na wenzako kulingana na mahitaji ya wakati huo hakikisha uwajibika vizuri.

Aidha tambueni uongozi wa kupenda kupokea maoni, umoja wetu na mshikamano wetu ndio msingi wa chama chetu, mtu yeyote kwa malalamiko yake akikuletea malalamiko ya kutugawanya mkatae anataka kuleta mafarakano na kugawa chama