Na Isri Mohamed

Baada ya Ivory Coast Kutwaa Ubingwa wa AFCON 2023 jina la Mchezaji Sébastien Haller Aliyefunga Bao la Ushindi Lililowapa Ubingwa Limetajwa sana kama shujaa wa Ivory Coast na rekodi yake na mwezi Februari..

Haller anaimbwa kama shujaa wa Ivory Coast kwa sababu ndiye aliyefunga bao la ushindi lililowapeleka kwenye Fainali ya AFCON, na jana amefunga tena dhidi ya Nigeria bao lililowapa Ubingwa wa Afrika.

Stori ya kuvutia zaidi ya mshambuliaji huyu wa Borrusia Dortmund ni rekodi yake na mwezi Februari…

Februari 2022 Aligundulika kuwa na Ugonjwa wa Saratani ya Tezi Dume Uliozima Matumaini yake ya Kurejea Uwanjani.

Februari 2023 Haller anarudi Tena Uwanjani Na Kuendelea kuitumikia klabu yake ya Borrusia Dortmunt aliyosajiliwa akitokea Ajax.

Februari tena 2024, Haller Anaiwezesha timu yake ya Taifa Ivory Coast kufuzu fainali ya AFCON wakiwatoa Senegal kwa kufunga bao la ushindi.

Februari 11, 2024 anafunga tena dakika ya 81, bao la ushindi dhidi ya Nigeria lililowapa Ubingwa Ivory Coast wa AFCON.

By Jamhuri