Aliuawa baada ya kupigwa risasi kwenye maandamano ya Chadema

Dar es Salaam. Chuo cha Usafirishaji cha Taifa (NIT) kimesema aliyepigwa risasi jana Februari 16, 2018 eneo la Mkwajuni jijini Dar es Salaam na kufariki dunia ni mwanafunzi wa chuo hicho.

Chuo hicho kimemtaja mwanafunzi huyo kuwa ni Akwilina Akwiline aliyekuwa anasoma shahada ya kwanza ya ununuzi na ugavi.

Leo, Februari 17, 2018, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amekiri mtu mmoja kupigwa risasi na polisi wakati wakiwatawanya wafuasi wa Chadema walioandamana jana.

5364 Total Views 2 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!