Matokeo ya awali ya uchaguzi wa ubunge Jimbo la Kinondoni yameanza kubandikwa nje ya vituo vya kupigia kura yakionyesha mgombea wa CCM, Maulid Mtulia akiongoza katika baadhi ya vituo.

Katika matokeo hayo, Mtulia anafuatiwa kwa karibu na mgombea wa Chadema, Salum Mwalimu huku wa CUF, Salum Rajab Juma akishika nafasi ya tatu lakini kwa tofauti kubwa ya kura.

Baadhi ya matokeo hayo ni kama ifuatavyo; kituo cha Mashuka namba mbili Kata ya Tandale, Mtulia amepata kura 45, Mwalimu 16 na mgombea wa CUF, Salum Juma kura 7 huku wagombea wengine tisa wa vyama vingine wakipata kura sifuri.

Katika kituo cha Shule ya Msingi Kijitonyama C3, Mtulia amepata kura 23, Mwalimu 24 huku mgombea wa CUF akipata kura 1 na Mohamed Majaliwa wa NRA kura 1. Kituo hicho kina wapigakura 373 ila waliopiga kura ni 49.

Kituo cha Kijitonyama C2, Mwalimu amepata kura 18, Mtulia 18 huku wagombea wengine wakipata sifuri.

Kituo cha kijitonyama Shule ya Msingi C1, Mtulia amepata kura 29, Mwalimu kura 34 na Juma wa CUF kura 1.

Kituo cha Ofisa Mtendaji wa Kata A-4, Kata ya Hananasifu Mtulia amepata kura 38, Mwalimu kura 29 na Juma 2.

Katika Kituo cha Ofisa Mtendaji wa Kata C2, Kata ya Hananasifu; Mwalimu amepata kura 43 na Mtulia kura 34.

Kituo cha Ofisa Mtendaji wa Kata B-1, Kata ya Hananasifu; Mtulia amepata kura 42, Mwalimu 32 huku wagombea wa CCK na TLP wakipata kura moja kila mmoja.

Kituo cha Ofisi ya Mtendaji wa Mtaa B4 kilichopo Kata ya Hananasifu; Mtulia amepata kura 31 na Mwalimu kura 37, Juma 1 na mgombea wa Tadea kura 1.

Kituo cha Kisutu A-2 Kata ya Hananasifu; Mtulia amepata kura 48, Mwalimu 39.

Kituo cha Ofisi ya Mtendaji Kisutu A-3 Kata ya Hananasifu, Mwalimu amepata kura 29 na Mtulia kura 32 huku Juma akipata kura 1.

Kituo cha Leaders Club Frat-3 Kata ya Kinondoni, Mtulia amepata kura 35, Mwalimu 27.

Kituo cha Ofisi ya Mtendaji Mtaa B-1 Kata ya Hananasif, Mtulia amepata kura 42 na Mwalimu kura 32.

Kituo cha Hananasif A1 Kata ya Kinondoni, Mtulia amepata kura 37, Mwalimu 23 na Juma 1.

Kituo cha Shule ya Msingi Kijitonyama Kata ya Kijitonyama Mwalimu amepata kura 19 sawa na Mtulia kura 19.

Kituo cha Ofisi ya Ardhi-2 Kata ya Kinondoni, Mwalimu amepata kura 23, Mtulia 19.

Kituo cha Shule ya Msingi Kijitonyama A-1, Mtulia kura 25, Mwalimu kura 35.

Kituo cha Idrisa 6 Kata ya Magomeni, Mtulia amepata kura 58, Mwalimu kura 21.

Kituo cha Idrisa 3 Kata ya Magomeni, Mwalimu amepata kura 180, Mwalimu kura 36 na Juma 3.

Kituo cha Idrisa 1 Kata ya Magomeni, Mtulia kura 26, Mwalimu kura 21 na Juma 3.

Kituo cha Idrisa 2 Kata ya Magomeni, Mtulia amepata kura 44, Mwalimu 23 na Juma 3.

Kituo cha Ofisi ya Aweo-5 Kata ya Makumbusho, Mtulia amepata kura 42, Mwalimu 20, Juma 2.

Kituo cha Weo Kata ya Makumbusho, Mtulia amepata kura 54, Mwalimu 36, Juma 1 na Johnson Mwangosi wa Sau 1.

Matokeo zaidi yataendelea kukujia hapahapa

Leo February 17. 2018 Wananchi wa Kinondoni  wamepiga Kura kuchagua Mbunge wa Jimbo hilo katika Uchaguzi Mdogo nakusogeze baadhi ya Matokeo ya Uchaguzi wa Mbunge katika baadhi ya Vituo cha kupiga kura kabla ya kutangazwa kwa kura za jumla.

Please follow and like us:
Pin Share