Home Michezo ARSENAL, CHELSEA ZASHINDWA KUTAMBIANA

ARSENAL, CHELSEA ZASHINDWA KUTAMBIANA

by Jamhuri

Mchezo mmoja wa ligi kuu Uingereza uliopigwa jana usiku uliwakutanisha timu mbili zinazotoka mji mmoja London, Arsenal na Chelsea zimeshindwa kutambiana baada ya kutoka sare ya mabao 2-2.

katika mchezo Chelsea ilipaswa kupata pointi zote tatu katika mechi hiyo kwani mpaka dakika 90 Chelsea ilikuwa mbele ya mabao 2-1 ambapo lakini dakika za nyongeza ya 92 Hector Bellerin alifuta ndoto za chelsea kuibuka na point tatu alipoisawazishia timu yake ya Arsenala na kuufanya mchezo uishe kwa mabao 2-2.

Mabao ya Arsenal yalifungwa na Jack Wilshere dakika ya 63 na Hector Bellerin dakika ya 92 huku yale ya Chelsea yalifungwa na Hazard kwa mkwaju wa penalti dakika 67, ambayo Arsene Wenger aliita “kichekesho”, na goli la pili lilifungwa na Marcos Alonso dakika ya 84.

Mchezo huo ulikuwa 50-50, timu zote zilicheza mchezo mzuri,” kwa matokeo hayo Chelsea wanabakia nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Premier League, pointi moja nyuma ya Manchester United inayoshika nafasi ya pili huku Arsenal ikibaki nafasi ya 6 na point zake 39.

You may also like