Home Michezo AZAM FC: HATUTAKUBALI KUFUNGWA MARA MBILI NA TIMU MOJA

AZAM FC: HATUTAKUBALI KUFUNGWA MARA MBILI NA TIMU MOJA

by Jamhuri

Licha ya kutinga fainali lakini kocha wa Azam Aristica Ciaoba amesema hiyo ni nafasi pekee ya kulipa kisasi cha kufungwa na URA mechi za makundi
Kocha Mkuu wa Azam FC, Aristica Cioaba, amesema anauhakika timu yake itatetea ubingwa wake wa Kombe la Mapinduzi kutokana na ari waliyokuwa
nao wachezaji wake.
Coaba amesema, anajua anakwenda kukutana na URA timu ambayo iliwafunga kwenye mchezo wa makundi hivyo walichopanga
ni kulipa kisasi na kutwaa ubingwa wao kama ilivyokuwa mwaka jana.
“Siwezi kuwaogopa URA wala kuwazarau lakini ninachojua Azam itateakombe lake, kwasababu hatutokubali kufungwa mara mbili na timu moja
mechi hiyo tumeipa uzito na tulichopanga ni kulipa kisasi na kuchukua kombe letu,”amesema Cioaba.
Kocha huyo hakusita kuwasifia wachezaji wake kwa mapambano waliyoonyesha kwenye mchezo huo wa nusu fainali dhidi ya Singida
United na kusema kitu hicho ndiyo kinampa matumaini ya kusema hivyo.
Fainali ya michuano hiyo imepangwa kufanyika Jumamosi kwenye uwanja huo wa Amaan majira ya saa 2:15 usiku ambapo ndipo bingwa wa 12 wa
michuano hiyo atakapo julikana.
Azam ilitinga fainali jana usiku baada ya kuwafunga Singida United bao 1-0, na kuiweka timu hiyo ya tajiri Salim Said Bakressa katika nafasi nzuri ya kutetea taji lake kwa mara ya pili.

You may also like