Na Severin Blasio,JamhuriMedia,Morogoro

Wakati jitihada za kukomesha ukatili wa kijinsia hususani kwa wanawake,zinaendea imeelezwa bado baadhi ya wanaume wamekuwa kikwazo katika kukwamisha na kuwakatisha tamaa wanawake.

Hayo yameelezwa kwenye mafunzo ya wanawake na makundi maalumu kutoka Kata za Bwakira juu,Selembala na Kisaki zilizopo Halmashauri ya Morogoro yaliyoandaliwa na asasi ya UMWEMA kwa kushirikiana na The Foundation for Civil Society FCS.

Afisa Mradi wa Umwema Morogoro akitoa elimu kwa wanawake na makundi maalum juu ya elimu ya Jinsia na Utatuzi wa Migogoro ya Ardhi yaliyofanyika Kisaki Gomerok atika Kata ya Kisaki Halmashauri ya Morogoro.

Wakizungumza kwenye mafunzo yaliyofanyika Kisaki Gomero washiriki wa mafunzo hao walitoa yao ya moyoni kuhusu changamoto zinazo wakabili wanawake majawapo ikiwa ni elimu kwa wanawake kutowafikia hususani wanawake wa vijijini sambaba na wanaume kutowapa ushirikiano pindi wanapotaka kupiga hatua .

Kwa nyakati tofauti washiriki wa mafunzo hayo walidai baadhi ya wanaume wanawakatisha tamaa wake zao wakitolea mfano wa mwanamke anapokuwa anafanya biashara na mme kuchukua pesa za biashara yake bila makubaliano na kuzitumia jambo linalorudisha nyuma maendeleo ya wanawake katika kujikwamua kiuchumi.

”Wanaume zetu wanatukatisha tama!Utakuta mwanamke anafanya biashara zake, mwanaume anaingilia kati zile pesa anachukua zote na kuzitumia nashindwa kuendelea maana mtaji kasha chukua” amesema Agness.

Awali Mratibu wa asasi ya Umwema Restuta Ngonyani amesema asasi hiyo imetoa mafunzo hayo kwa lengo la kuwafanya wanawake na makundi maalumu waweze kutumia rasilimali walizonazo katika kujikwamua kiuchumi.

Mshiriki wa Mafunzo Grace Maregesi akiwasilisha kazi ya kikundi baada ya Mafunzo

Restuta pamoja na mambo mengine aliwataka washiriki wa mafunzo hayo kuwa mabalozi wa wanawake ambao hawakupata fursa hiyo kwa ili kuondokana na kuwa tegemezi.

Aidha aliwataka wanawake hao kuunda majukwaa yatakaowasaidia kukutana mara kwa mara kwa ajili ya kujadili suala la maendeleo yao.

“Baada ya mafunzo haya nendeni mkawe mabalozi wazuri kwa wanawake wenzenu ambao hawakupata fursa hii.mkaaanzishe majukwaa ya wanawake ambayo yatasaidia kuhamasisha wanawake wengikwa lengo la kujitambua,katika kumiliki ardhi kwa ajili ya kuepuka migogoro inayo wakumba katika jamiizenu” amesema.

Naye mkuu wa kitengo cha dawati la jinsia Jeshi la Polisi kituo cha Kisaki CCP Mangu alipata fursa ya kutoa elimu juu ya ukatili wa kijinsia kwa washiriki wa mafunzo hayo.

Katika mafunzo hayo CCP Mangu alisema jeshi hilo limeanzisha mpango wa kupambana na ukatili wa kijinsia majumbani sambamba na utoaji elimu kwa jamii na kuwataka wanawake kutoa ushirikiano katika kufichua makosa hayo.

Polisi Kata ,wa kwanza kulia akitoa maelekezo jinsi walivyojipanga kutokomeza ukatili wa kijinsia na migogoro ya ardhi baina ya wakulima na wafugaji
Please follow and like us:
Pin Share