Amani Martin mkazi wa Kata ya Nzihi Halmashauri ya Wilaya ya Iringa anashikiliwa na Jeshi la Polisi tuhuma za kumlawiti mtoto wake wa kumzaa mwenye umri wa mwaka mmoja na kumsababishia maumivu makali.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa Allan Bukumbi amesema mbinu aliyotumia mtuhumiwa ni kumshika mtoto kwa nguvu na kumfanyia kitendo hicho wakati wakiwa shambani baada ya mama wa mtoto kuondoka kwenda kuokota kuni na kumuacha mtoto akiwa na baba yake

Kamanda Bukumbi amesema kiini cha tukio hilo bado kinachunguzwa na mtuhumiwa amekamatwa na taratibu za kisheria zinaendelea kuchukuliwa dhidi yake

Wakati huo huo,Jeshi la Polisi mkoani Iringa linawashikilia watuhumiwa watatu kwa makosa ya kumiliki silaha kinyume na utaratibu katika maeneo tofauti ya mkoa huo huku baadhi yao wakikodisha silaha hizo kwa watu kinyume na sheria.

By Jamhuri