Na Dotto Kwilasa, JamhuriMedia, Dodoma

Serikali imewasilisha bajeti yake kuu kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 huku ikianisha vipaumbele mbalimbali ikiwemo kuondoa ada kwa wanafunzi wa kidato cha nne ambao watakuwa wakichaguliwa kujiunga na Vyuo vya ufundi pamoja na kuondoa kodi na tozo katika bidhaa na huduma mbalimbali nchini.

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.Mwigulu Nchemba amewasilisha bajeti hiyo leo June 15,2023 Bungeni na kuagiza kuanzia Julai Mosi Mwaka 2023 maeneo yote ya uzalishaji yasifungwe kwa kigezo cha kukiuka utaratibu na kuitaka Mamlaka ya ukusanyaji mapato Tanzania TRA kukusanya Kodi kwa kufuata kanuni..

Amesema,Serikali inatarajia kutekeleza miradi mbalimbali ya mendeleo ikiwemo kujenga mabwawa na hivyo inatarajia kukusanya na kutumia jumla ya Trilioni 44.39 kwa Mwaka wa fedha 2023/2024

Waziri huyo wa Fedha amebainisha kuwa makadirio ya Bajeti ya Serikali kwa mwakawa fedha 2023/24 yameandaliwa kwa kuzingatia nyaraka na miongozo mbalimbali ya kitaifa na kimataifa .

“Makadilio haya yamezingaa mpango wa tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano kuanzia 2021/22-2025/26 ambao umezingatia Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 ,ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020 na Dira ya Maendeleo ya Afrika Mashariki 2050,”amesema

Miongozo mingine ni Ajenda ya Maendeleo ya Afrika 2063,malengo ya Maendeleo Endelevu 2030,mwongozo wa Ushirikiano wa Maendeleo endelevu wa Umoja wa Mataifa wa mwaka 2022 -2022 na makubaliano mengine ya kikanda na kimataifa ambayo Tanzania imeridhia; na hotuba mbalimbali za Mheshimiwa Rais.

Pamoja na hayo amesema Serikali imeonesha nia na jitihada kubwa katika kuboresha Utumishi wa Umma nchini kwa kuzingatia sera, sheria, kanuni na miongozo iliyopo na kwamba kutokana na jitihada hizo mafanikio mengi yamepatikana.

Ameyataja mafanikio hayo kuwa ni pamoja na kupandisha madaraja watumishi 135,170 wenye sifa stahiki ambapo hadi Aprili
2023, jumla ya shilingi bilioni 177.9 zimetumika.

Mafanikio mengine ni kuongeza mishahara ya watumishi wa umma, ambapo kima cha chini cha mishahara kiliongezeka kutoka shilingi 300,000 hadi shilingi 370,000 na kulipa madeni ya malimbikizo ya mishahara kwa Watumishi wa Umma 94,290yenye thamani ya shilingi bilioni 165.9hadi Aprili2023.

“Kwa kipindi kifupi Cha awamu ya Sita mafanikio mengi yamepatikana ikiwemo kupunguza kodi ya mapato ya ajira (PAYE)
kutoka asilimia 9 hadi asilimia 8,kuondoa tozo ya limbikizo la Mkopo wa Elimu ya Juu, ambapo takribani kiasi cha shilingi trilioni 1.1 kilisamehewa na kulipa madeni ya watumishi (yasiyo ya kimshahara) shilingi bilioni42.7 hadi 36,”amefafanua.

By Jamhuri