Canada imetangaza kumfukuza balozi wa Venezuela Wilmer Barrientos Fernández

Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni Chrystia Freeland alisema hatua hiyo ni jibu kwa kufukuzwa kwa mwanadiplomasia wake wa cheo cha juu kutoka Venezuela mwishoni mwa wiki.

Venezuela iliilaumu Canada kwa kuingilia masuala yake ya ndani.

Cadana ilikuwa imeilaumu serikali ya Rais Nicholas Maduro kwa ukiuja wa haki za binadamu.

Zaidi ya watu 120 wameuawa wakati wa miezi kadha ya kuipinga serikali mapema mwaka huu.

Bi Freeland alisema kuwa Bw. Barrientos alikuwa tayari nje ya nchi na hataruhusiwa kurudi Cnada huku afisa mwingine wa kibalozi naye akitakiwa kuondoka.

Canada tayari ilikuwa imewawekea vikwazo maafisa wa vyeo vya juu wa Venezuela katika hatua ambayo iliikasirisha serikali ya Venezuela.

Venezuela pia ilimfukuza balozi wa Brazil Ruy Pereira, kutokana na madai kuwa serikali yake imekiuka sheria.

By Jamhuri