BASATA: Hatupo kwa ajili ya kufungia kazi ya msanii

Na Mwandishi Wetu,JamhuriMedia,Dar

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA),limewakumbusha wasanii kuwa hawana lengo la kufungia kazi ya msanii bali wapo Kwa ajili ya kuzungumza na kurekebisha kazi ili kuikuza tasnia ya Sanaa kwa mapana.

Akizungumza kauli hiyo Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Dkt.Kedmon Mapana wakati wa kuwapa nasaha na baraka pamoja na kupokea maoni yao huku akiwakabidhi bendera washiriki wa tuzo za zikomo zilizowajumuisha wasani wa filamu,wabunifu wa mavazi,wasanii wa vichekesho, watangazaji,wapiga Muziki ambao wanatajiwa kwenda nchini Zambia kwa ajili ya kilele cha fainali hiyo inayotarajiwa kufanyika rasmi mwezi octoba Jijini Lusaka nchini Zambia.

Mapana amefafanua zaidi kuwa kwa sasa Watanzania wawapigie kura nyingi washiriki hao ambao kwa upande wa Tanzania tunagombea tuzo 50 katika vipengele tofauti tofauti.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Dkt.Kedmon Mapana akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 19,2022  Jijini Dar es Salaam wakati wa kuwapa nasaha na baraka pamoja na kupokea maoni yao Huku akiwakabidhi bendera washiriki wa tuzo za zikomo zilizowajumuisha wasani wa Filamu, wabunifu wa Mavazi,wasanii wa vichekesho, watangazaji,wapiga Muziki ambao wanatajiwa kwenda nchini Zambia kwa ajili ya kilele cha fainali hiyo inayotarajiwa kufanyika rasmi mwezi octoba Jijini Lusaka nchini Zambia.

“Watakaoshiriki wote tutawapatia vyeti vya kutambulika mchango wao katika ushiriki wao na kwa washindi pia watapewa zawadi hivyo tutawaandalia usiku wao wa kuwapongeza Ili waweze kuona basata sio sehemu ya kuwafungia tu kazi zao au kutoa vibali bali pia no sehemu ya kuchagiza na kutoa hamasa pale taifa linapokua nje kwenye vinyang’anyiro vya tuzo za Kimataifa,” amesema .

Hata hivyo Mapana amesisitiza zaidi kuwa wasanii wanatakiwa kujisajiri BASATA ili waweze kupata fursa na vipaumbele mbalimbali vinavyotokea ikiwemo kupatiwa mikopo kwa wasani ambao kigezo cha kwanza ni kutambulika kisheria.

Kwa upande wake mbunifu wa mavazi nchini Martin Kadinda amewaomba BASATA kuwashika mkono katika safari ya kuelekea zambia Kwa upande wa usafiri ili washiriki waweze kumudu kusafiri ili kupata hamasa zaidi na kurudi na ushindi wao.