Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam (RC),Amos Makala amesema kuwa katika operesheni imewakamata wahalifu 135 pamoja na vitu mbalimbali vya wizi ikiwemo runinga 23.

Akizungumza leo Septemba 19, 2022 jijini Dar es Salaam, amesema kuwa watuhumiwa hao wamekamatwa katika ndani ya siku nne tangu kuanza kwa operesheni ya kuzuia uhalifu iliyoanza Septemba 15,2022.

Makala amesema wengi waliokamatwa vijana wenye umri kati ya miaka 14 na 30 walibainika kuhusika na matukio ya uvamizi mitaani maarufu kama Panya Road.

Amesema kuwa katika mahojiano ilibainika viongozi wa magenge hayo baadhi yao waliwahi kutumikia vifungo mbalimbali magerezani.

“Wamekamatwa pia wanunuzi wakubwa watano wa bidhaa za wizi,” amesema Makala”