Na Mwandishi Wetu, Jamhuri Media, Dar Es Salaam

Waziri wa Kilimo Hussein Mohamed Bashe amewakaribisha wageni kutoka mataifa mbalimbali kuja kuwekeza katika kilimo nchini Tanzania na kubainisha vipaumbele lukuki vilivyopo katika sekta hiyo.

Mhe. Hussein Bashe (Mb), Waziri wa Kilimo akiwasilisha kwenye Jukwaa la majadiliano kuhusu vipaumbele vya Sekta ya Kilimo ambapo ametumia nafasi hiyo kuhamasisha wageni kutoka Mataifa mbalimbali Duniani kuwekeza kwa wingi Tanzania ili kunufaika na fursa zinazopatokana katika Sekta ya Kilimo.

 Majadiliano hayo pia yamehusisha viongozi mbalimbali akiwemo Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda, Waziri wa Fedha, Mhe. Mwigulu Nchemba (Mb), Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (Mb), Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji Mifugo, Maliasili – Zanzibar Mhe.Shamata Shahame Khamis (Mb), na Waziri wa Uchumi wa Buluu – Zanzibar Mhe. Suleiman Masoud Makame (Mb).Mhe. Waziri Bashe ameongea hayo wakati wa kikao cha pembezoni mwa Mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika (AGRF 2023) ulioanza leo tarehe 5 Septemba 2023, katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.