Basi la abiria lateketea kwa moto Kigoma

Basi la Kampuni ya Saratoga lenye namba za usajili T476 ADG lililokuwa likitoka mkoani Kigoma kwenda Sumbawanga limeteketea kwa moto eneo la Kijiji cha Kazuramimba mkoani Kigoma.

Jeshi la Polisi kupitia kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, ACP Martin Ottieno limesema kuwa bado linachunguza chanzo cha moto huo.

Kwa mujibu wa Kamanda huyo, abiria wote wametoka salama na baadhi ya mizigo imeokolewa.

 

3542 Total Views 2 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!
Tags :
Show Buttons
Hide Buttons