Bei ya mafuta ya petroli na dizeli ya mwezi Oktoba imepungua ambapo kwa Mkoa wa Dar es Salaam petroli itauzwa kwa Sh.2886 huku dizeli ikiuzwa kwa Sh. 3,083 kwa bei ya rejareja

Kwa mkoa wa Tanga Petrol itauzwa 2,924 na Dizel itauzwa 3,108 huku kwa mkoa wa Mtwara Petrol otauzwa 2,908 na Dizel itauzwa 3,099

Taarifa ya EWURA imeeleza kuwa kushuka kwa bei za mafuta kumetokana na kushuka kwa bei ya bidhaa hizo katika soko la dunia kwa Agosti 2022, ambazo zimetumika katika kukokotoa bei za mafuta za hapa nchini katika mwezi wa Oktoba 2022 zimepungua kwa asilimia 7.4, 3.9 na 1.9 kwa mafuta ya petroli, dizeli na mafuta ya taa, mtawalia, ikilinganishwa na bei hizo kwa mwezi Julai 2022