Benki Kuu ya Tanzania imeendelea kushiriki kikamilifu katika Soko la Jumla la Fedha za Kigeni, kwa kuuza dola ya Marekani kwa benki za biashara ikiwa ni sehemu ya juhudi zinazoendelea za kupunguza uhaba wa fedha za kigeni nchini.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) iliyotolew Machi 23, 2-024 imesema, Mpango huu unalenga kuhakikisha kuna ukwasi wa kutosha wa fedha za kigeni katika soko.

Taarifa hiyo imesema, mpango huu unalenga kuhakikisha kuwa wananchi wenye uhitaji halali wa fedha za kigeni wanapata huduma hiyo kwa bei ya soko kupitia Taasisi rasmi za fedha nchini.

“Ni muhimu kwa wadau wote kuelewa kuwa ushiriki wa Benki Kuu ya Tanzania katika Soko la Jumla la Fedha za Kigeni unazingatia Sera ya Ushiriki katika Soko la Fedha za Kigeni (Foreign Exchange Intervention Policy) yenye lengo la kukuza utulivu wa soko na kukidhi mahitaji halali ya fedha za kigeni nchini.” Taarifa hiyo imefafanua.